156 Bwana Yesu yuko wapi

1. Bwana Yesu yuko wapi, Mpenzi wangu rafiki? Njia gani amekwenda? Nitamwonaje mimi? Roho yangu yajutishwa Na dhambi na huzuni; Yesu mpenzi wangu Mwema Namtafuta kwa bidii.   

2. Ninapaza sauti yangu Nalia:wapi Yesu? Ndani mwangu sina raha Mpaka nimwone Yesu. Ningekuwa na mabawa Ningeruka upesi Milimani, mabondeni Kumtafuta Bwanangu   

3. Aondoa shida zangu, Maharibifu yote. Nikiona taabu mimi Anituliza yeye. Nitafanya bidii sana; Kumtafuta popote; Sitachoka kutembea Mchana hata usiku.   

4. Bwana Yesu nitokee, Roho inakuita. Niondoe na maovu Yesu mwokozi wangu. Utilize hamu yangu Kaa kwangu daima. Nikupende sana wewe, Niwe wako milele.  


Comments

Popular posts from this blog

157 Kijito cha utakaso

155 Hapana rafiki kama Yesu

153 Nimepita ulimwengu